Ugali Sosa

July 06, 2010 at 00:13

LISTEN TO ‘UGALI SOSA’

Artist: Man Ingwe
Song: Ugali Sosa
Album: Ugali Sosa
Year: 2010
Producer: Bizi B
Record Label: Lampstand Records
Language: Kiswahili

Chorus
natafuta Mfalme wa Mungu
na utakatifu, wake
na vitu vyote vile vizuri
nitaongezewa kama ugali sosa

huwezi pewa
ugali sosa
kama bado
hujanunua
basi mwenzangu mtafute Mungu
utaongezewa
ugali sosa

Verse 1
kuna hoteli ambao mi huenda
kukamata ugali na supu ya magoti
mara tu mlima wa ugali ukifika
naanza kufanya testi za mluhya
ya kwanza nafinya ugali
inachomoka pande zote za mkono
ya pili navumba ugali
tupa kwa ukuta
narudi kama tennis
ya tatu napuliza ugali
na moshi nyeupe inaenda spiral
ugali inapata certificate
waiter, leta sosa!

Chorus
natafuta Mfalme wa Mungu
na utakatifu, wake
na vitu vyote vile vizuri
nitaongezewa kama ugali sosa

huwezi pewa
ugali sosa
kama bado
hujanunua
basi mwenzangu mtafute Mungu
utaongezewa
ugali sosa

Verse 2
naanza kusakata ugali
naweka ugali hapo kwa angle theta
alafu na mwana Wepukhulu
kumbe alikuwa pande kwa ile meza
waiter anamkaribia
anamuuliza nikupe nini bwana
Wepukhulu anasema “ugali sosa na kadhalika”
waiter anasema “excuse me”
Wepukhulu anazusha
ma-bouncer wakambeba juu
wakamtandika, chonga viazi

Chorus
natafuta Mfalme wa Mungu
na utakatifu, wake
na vitu vyote vile vizuri
nitaongezewa kama ugali sosa

huwezi pewa
ugali sosa
kama bado
hujanunua
basi mwenzangu mtafute Mungu
utaongezewa
ugali sosa

Verse 3
sasa wasee iko hivi
tabia mbaya lazima tutawacha
tunataka baraka zake Mungu
lakini tunakataa Mungu mwenye baraka
tunataka tupate uponyaji
lakini tunakataa Yesu mwenye kuponya
tunapenda sana miujiza
lakini hatupendi Mungu mwenye kutenda
ni lazima tutatubu wapendwa
tubadili mienendo tumtafute Mungu
ukidharau mambo hii nasema
haki roho safi
utachonga viazi

Chorus
natafuta Mfalme wa Mungu
na utakatifu, wake
na vitu vyote vile vizuri
nitaongezewa kama ugali sosa

huwezi pewa
ugali sosa
kama bado
hujanunua
basi mwenzangu mtafute Mungu
utaongezewa
ugali sosa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in