Loading...

County Boy aeleza mipango yake ya kuwa kutanisha Alikiba na Diamond Platnumz

July 14, 2017 at 15:08
County Boy aeleza mipango yake ya kuwa kutanisha Alikiba na Diamond Platnumz

Mwananziki Country Boy kutoka Tanzania amefunguka kudai kuwa ana mipango ya kuwakutanisha Diamond Platnumz na Alikiba – kitu ambacho tunajua ni ngumu kufanyika.

Msanii huyu akizungumza na Daladala Beat ya Magic Fm alidai kuwa kwa hivi sasa anataka kuwashirikisha wasanii hawa kwa wimbo wake mpya, huku akitarajia kuwa watasikizana. Country Boy alisema;

“Round hii nataka nilete different sound kwa sababu tayari am rapper nataka nitengeneze sound mpya. Nawataka hawa malegendary wawili, hapa Alikiba, hapa Diamond ila siwashirikishi katika track moja, kila mtu na ngoma yake,”

Aliendelea kwa kusema…

“Kila mtu na upande wake natengeneza sound mpya, nahisi nitaleta kitu kikubwa. Ninachoshukuru kwa Mungu mimi nipo flexible naweza kurap katika beat yoyote,”

Hata hivyo wacha tuone Kama Country Boy ataweza kufanya hivi.


in Entertainment
Loading...

I write entertainment stories as well review and critic local music. Apart from my busy schedule you can catch me on my IG: @I_am_kermbua and Facebook: Lyne Syombua.