Aisha Asema Neno Kuhusu Watoto Walioshinda Tuzo za SZIFF

Mwanadada mkongwe katika ukuaji wa sanaa hasa ya filamu nchini,  AISHA kutoka kundi la siku nyingi la maigizo la MAMBO HAYO, amefunguka na kutia neno katika tuzo za filamu Tanzania zilizotolewa wikiendi iliyopita zikiwa zimeandaliwa na AZAM TV.

Aisha anasema kuwa pamoja na kwamba wanalengo la kukuza vipaji lakini wamekosea sana kuwapa TUZO hizo watoto wadogo ambao ni wasanii wachanga na hata vipaji vyao bado havionekani kama vinaweza kushindwanisha na wasanii kama Wema sepetu , Gabo na hata Monalisa kama walivyofanya.

download latest music    

Aisha kutoka mambo hayo aliandika kwa kusema ”

Nimetoka kuangalia sinema zetu! Nilibahatika kuiona kidogo Filamu ya kesho! Msema kweli mpenzi wa Mungu watoto walioshinda kwenye uigizaji bado kabisa! Wanajikanyaga mno! Bado hawajakomaa kabisaa!! Kwenye uchezaji!! Hata mai zumo ni bora Mara Mia! Kuwapa ushindi dhidi ya wema, Monalisa, gabo , johari, phd na wengine ? sijui ni vigezo vipi wametumia! Kama ni kura tu ni kura zipi zilizopigwa kuwazidi wakongwe waliokuwa wanapigiwa usiku na mchana? Je hawa watoto wapo nyuma ya Nani? Nani kafanya hili deal litiki? Mimi ile naiita Aibu ya mwaka! Ni Aibu kubwa sana sana kwenye tunzo za sinema zetu! Yaani uigizaji ule ndio uwafanye wewe bora? Wenzetu wa Kenya, Uganda, nigeria wakibahatika kuiona filam ya kesho na kuwaona wale watoto wanavyoigiza eti ndio waigizaji bora si Aibu hii jamani? Hiki ni kichekesho kilichopitiliza kwa kweli! (hayo ni mawazo yangu tu mhenga Mimi)nimeudhika mpaka nimetoa povu Leo!”

Wasanii wengi wamelalamika sana kuhusu Tuzo hizo wa sababu wasanii waliopata tuzo hizo hawakutegemewa wala kujulikana katika tasnia ya filamu nchini na hata kazi yao haijajulikana sana kama ilivyokuwa ikitegemewa .

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.