Ali Kiba Afunguka Baada Ya Kumzika Baba Yake

Staa wa muziki wa Bongo fleva Ali Saleh Kiba amefunguka Baada ya kumzika baba yake mzazi aliyefariki siku ya jana.

Baba mzazi wa Ali Kiba na ndugu zake Abdu Kiba na Zabibu Kiba alifanikiwa Dubai siku ya jana kutokana na maradhi ya moyo ambayo yalizuka yanasemekana kumuandama kwa siku nyingi.

download latest music    

Mzee Saleh alizikwa siku ya jana katika makaburi ya Kisutu ambapo Maelfu ya watu wamiminika katika mitaa ya Kariakoo kwa ajili ya kumsindikiza baba mzazi wa msanii Alikiba ambaye amepoteza maisha.

Baada ya kumzika Baba Yake hatimaye Ali Kiba amefungukia msiba huo uliompata yeye na famili yake na kuandika maneno haya Kupitia ukurasa wake wa Instagram:

Nawashukuru wote walioshiriki katika mazishi ya Mzee wangu, Na wale ambao hawakujaaliwa pia mimi na familia yangu tumefarijika sana Namuomba Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi na atupe subira katika kipindi hiki kigumu”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.