Ali Kiba Akumbwa na Tuhuma Nzito Za Wizi

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Ali Kiba amejikuta katika kitimoto Baada ya Msanii mkongwe wa Bongo fleva Domo Kaya kumtuhumu msanii huyo kwa wizi.

Tuhuma hizo zimekuja Baada ya Ali Kiba kutoa wimbo wake unaofanya vizuri hivi sasa ‘Kadogo’ ambapo ndani ya wimbo huo anasikika akitumia kidokezo cha ‘Yebaba’ ambacho Domokaya amedai amebuni yeye.

download latest music    

Domo Kaya amemuibukia Ali Kiba na kuwataka wasanii wengine wote hasa wapya kwenye tasnia ya Bongo fleva kuwa wabunifu kwenye kazi zao na sio kutegemea ubunifu wa wengine.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Friday Night Live cha East Africa Tv, Domo Kaya amesema kuwa haikuwa Vibaya kwa Ali Kiba kutumia neno hilo Lakini kiukweli alitakiwa kumuomba ruhusa kwanza:

Nawasihi wadogo zetu kuwa wabunifu na kuacha ujanja ujanja maana kutumia kitu hukatazwi Lakini uombe kwa muhusika akupe baraka”.

Wimbo wa Kadogo wa Ali Kiba unaendelea kufanya vizuri na kumpa chati Msanii huyo.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.