Ali Kiba Kupiga Shoo na Yvonne Chakachaka

Mwanamuziki katika tasnia ya Bongo movie Ali Kiba amefunguka kwamba atafanya shoo mbili za kufanga mwaka jijini Dar es Salaam ambapo atakuwa na muimbaji mkongwe, Yvonne Chakachaka kutoka Afrika Kusini.

Kupitia ukurasa wa Instagram, Ali Kiba amesema atafanya shoo hizo kabla ya mwaka haujaisha:

download latest music    

Ikiwa leo ni siku yangu ya kuzaliwa namshukuru Mungu kwa kuendelea kunibariki katika kila jambo na namshukuru kwa kunipa mashabiki wanaonipa support ya dhati kabisa. Shukrani zangu kwa mashabiki mwaka huu katika Funga mwaka na King Kiba zinakuja na show mbili kubwa ndani ya Desemba 2018.

1st Edition ya Funga Mwaka Na King Kiba nitakuwa na Princess of Africa Mama Yvonne_ ChakaChaka itafanyika Serena Hotel Dar es Salaam 22. December. 2018. Halafu 2nd Edition ya Funga Mwaka Na KingKiba itatukutanisha pale Next Door Arena, Dar es Salaam tarehe 29. December.2018.”

Hii haikuwa mara ya kwanza Msanii kwa Ali Kiba kumleta Yvonne Chakachaka na kupiga naye shoo, ameshawahi kumleta na Kuperfom naye katika siku ya wanawake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.