Alichojibu Nyandu Tozzy Kuhusu Kolabo na Harmonize.

Msanii wa muziki Bongo, Nyandu Tozzy amefunguka kuhusu mipango ya kufanya kolabo na Harmonize.
Nyandu Tozzy ambaye anafanya vizuri na wimbo mpya ‘I don’t care’ amesema kuwa kutokana na ukaribu wao lolote linaweza kutokea lakini bado hawajakaa na kuzungumzia hilo.

Unajua kwanza naweze kusema mimi na Harmonize ni wana ambao hatuwezi kukaa wiki mbili hatujawasiliana, so naweza kusema ni mdogo wangu kwenye huu muziki. Hivyo usishangae chochote kikatoka baina yangu mimi na yeye,” Nyandu ameiambia The Playlist ya Times FM.

download latest music    

Nyandu Tozzy amekuwa akitumbuiza kwenye show kadhaa ambazo Harmonize amekuwa akiziandaa ikiwemo ile aliyofanya Dar Live mwaka huu.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.