Alichosema Chid Benz Kuhusu Mh Makonda

Msanii wa muziki Chid Benz amefunguka  na kuandika ujumbe mzito kwa mh mkuu wa mkoa wa jijini Dar es salaam kwa kusema kuwa mkuu wa mkoa huyo anatakiwa aachane na mambo ya muziki na wasanii na kudeal na mambo ya serikali sio kukaa kufanya vitu kwa kuichanganya serikali.

Chid benz anasema kuwa inawezekana kuwa makonda akawa na moyo wa kufanya yote kwa ajili ya watu wa Dar lakini nguvu ya kufanya hivyo hana kwa sababu yuko na mambo mengi ya kufanya hivyo anawez kupata lawama kutokana na yale anayoyafanya.

download latest music    

Chid benz anasema kuna mamb mengi ya kufanya katika jamii ukiachilia mbali na yale anayoyafanywa kwa sasa kwa wasanii .

Chid benz anasema kuwa mh makonda aache kutafuta kupigiwa kelele na wasanii badala yake aangalie mambo muhimu ya kufanya katika jamii kama kuleta madawa katika mahospitali, ukarabati wa vituo vya daladala  ili kupunguza lawama kwa wananchi.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.