Alichosema Mamake Hamisa Mobeto baada ya Zari Hassan kumtolea mwanawe povu

Image: Mama Hamisa

Maneno yamemfika kooni mamake model Hamisa Mobeto baada ya picha kusambaa mitandaoni ikidaiwa bintiye amechora tatuu ya Diamond Platnumz.

Picha hiyo ilizua kero ikuluni,Madale kwa Diamond Platnumz na mpenzi wake Zari Hassan,hadi matusi na maneno yakaporomoshwa kumchafua Hamisa Mobeto.

download latest music    
Hamisa Mobetto
Hamisa Mobetto

Kuhusu stori hii, mamake Mobeto ameshindwa kujizuia.Na inasemekana amejikuta ashamtolea povu hatari sana Zari Hassan kwa sababu ya matusi aliyomtunukia Hamisa.

Akizungumza na gazeti la Global Publishers,mamake Mobeto alisema,’hakuna wakati mgumu kama kuona mtoto wake huyo anazungumziwa vibaya kila wakati katika mitandao ambapo wakati mwingine siyo jambo la kweli zaidi ya kumchafua tu.

Hamisa, Diamond na Zari
Hamisa, Diamond na Zari

Jamani mimi kama mzazi, sidhani kama kuna mzazi yeyote anayeweza kuvumilia kuona mwanaye kila mara yuko kwenye midomo ya watu au kuongelewa vibaya kwenye mitandao ya kijamii kwa vitu ambavyo hajafanya,” alisema.

“Unajua unapomuona Hamisa (Mobeto) amenyamaza, kila wakati wanatafuta kumuwekea jambo baya, kitu ambacho siyo sahihi, mimi sijawahi kuiona hiyo tatuu wanayosema zaidi ya kuona kuwa wanampandikizia maneno tu ya kumchafua, sipendezwi kabisa na tabia hiyo,” amemalizia huku akiwa na uchungu mwingi.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua