Alikiba afunguka kuhusu Diamond na yeye kuachia nyimbo siku moja

Alikiba aliachia wimbo wake ‘Seduce Me’ Agosti 25, siku hio hio Diamond pia aliwachia ‘Zilipendwa’ – wimbo ambayo aliwashirikisha wasanii wote wa Wasafi.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio jana Agosti 28, Alikiba alieleza kuwa wasanii kuingiliana kwenye ratiba kunashababishwa na kukosekana kwa umoja baina ya wasanii.

download latest music    

Kiba alisema kuwa wasanii wengi Bongo wanafanya muziki kama ushindani, alieleza kuwa yeye huachia nyimbo zake bila ya kufikiria mtu atoe wimbo ndo yeye pia atoe ngoma yake.

“Mimi kwa jinsi ninavyoona, naona kama ni sawa tu ni kwa sababu kukosekana kwa umoja unajua hata wenzetu (Wasanii wa nje) wanashauriana ili wasaidiane kusapoti na kuachiana nafasi ila kwa mimi sijaona kama kuna chochote kwa sababu umoja hakuna, hakuna umoja na watu wanafanya muziki kama ushindani, mimi huwa sifanyi hivyo…naachia ngoma zangu kwa ratiba sikufikiria mtu atoe nyimbo na mimi ndiyo nitoe ngoma,” alisema Alikiba.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere