Alikiba Amkumbuka Lulu, Mashabiki Wamshambulia.

Siku chache zilizopita msanii wa muziki wa bongo fleva King Kiba aliweka picha ya msanii wa bongo movies Lulu Michael ambae kwa sasa yupo gerezani akitumikia kifngo chake bila kuandika kitu chochote katika ukurasa wake wa Instagram.Hata hivyo inasemekana kuwa ni baada ya Alikiba kushindwa kuvumilia na kuamua kuonyesha hisia zake kuwa amem-miss msanii huyo.

Kwa Alikiba inaweza kuwa relief kwake lakini hali imekuwa tofauti kwa mashabiki ambao walianza kumshambulia msanii huyo na kumwambia kuwa ameanza kutafuta kiki kupitia mwanamke huyo ambae watu walimshambulia na kumwambia kuwa alikuwa nae katika mahusiano kwa muda mrefu  na amemkumbuka mwanamke huyo.

download latest music    

Baadhi ya msshabiki waliokuwa wakimshambulia walimwambia kuwa aachane na kiki na afanye kazi , hasitegemee kupata umaarufu kupitia picha ya lulu, huku wengine wakimwambia kuwa haisaidii kitu kuweka picha ya mtu aliye gerezani  na kuacha kuandika neno hata moja.

Lulu na Alikiba walikuwa watu wa karibu sana kipindi cha nyuma huku ikisemekana kuwa wawili hao walikuwa na uhusiano wa mapenzi lakini ulikuja kuvunjika.

Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela na ndicho anachokitumika sasa hivi baada ya kukutwa nahatia ya kuua bila kukusudia na kusababisha kifo cha aliekuwa mpenzi wake marehemu Steven Kanumba.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.