Loading...

Alikiba Namuona Kama Mtoto Wangu wa Kiume:-Vyonne Chakachaka

May 16, 2018 at 11:43
Alikiba Namuona Kama Mtoto Wangu wa Kiume:-Vyonne Chakachaka

Mwanamuziki mkongwe kutoka Afrika ya Kusini Vyonne Chakachaka amefunguka na kuelezea ukaribu wake na msanii wa bongo Alikiba ambae kipindi cha nyuma kidogo walishawahi kuonekana kuwa pamoja wakiwa studio na kusemekana kuwa walikuwa wakitengeneza nyimbo mpya ya pamoja.

Vyonne ambae hivi sasa yupo tanzania aliwahi kufanya mahojiano leo katika kipindi cha Clouds 360 katika clouds media na kuongea mengi lakini  hakusita kusema kuwa alikiba ni kama mwane wa kiume na meneja wa alikiba ambae ni Seven Mosha ni kma mtoto wake wa kike.

Loading...

Namuona alikiba kama mwanangu wa kiume na meneja wake ni kama mtoto wake wa kike, ninawapenda sana watoto wangu. na katika album yangu mpya inayokuja kuna wimbo nimeimba na alikiba na tuta-perform hivi kesho kwa mara ya kwanza.

Siku ya kesho mwanamama Vyonne ataperform katika mkutana wa Africa Connect ambapo kwa mara ya kwanza wataimba wimbo wa pamoja na Alikiba kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…