Amber Lulu Afunguka Baada Ya Kupata Ajali Mbaya

Image: Amber Lulu

Video vixen na msanii wa Bongo fleva mrembo Lulu Eugen maarufu kama Amber Lulu amefunguka mara baada ya kunusurika kifo baada ya kupata ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia jana.

Siku ya jana Amber lulu aliweka wazi kuhusu ajali mbaya ya gari iliyomkuta ingawa alikiri kupata majeraha kidogo lakini uoga alioupata ulikuwa mkubwa zaidi.

download latest music    

Kwenye exclusive interview na Global Publishers, Amber Lulu amefunguka kuwa anamshukuru Mungu kwa kuwa ametoka salama kwenye ajali hiyo iliyotokea juzi kati usiku wakiwa njiani kuelekea katika siku ya kuzaliwa ya msanii mwenzao, Messen Selekta.

Kwa kweli ilikuwa ajali mbaya sana, kwa sababu hata ukiiangalia gari tuliyokuwa tumepanda huwezi kuamini kama kuna watu wamepona, imeharibika vibaya, namshukuru sana Mungu kwa sababu nimetoka salama japo nina jeraha dogo mkononi”.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.