Amber Lulu Alilia Penzi la Prezzo, Haamini Kama Amemwagwa.

Msanii wa muziki anafanya vizuri katika muziki Amber Lulu ameonyeshwa kusikitishwa na habari zinazoendelea kutambaa kuwa mpenzi wake wasasa  ambae ni msanii mkubwa kutoka Kenya amemmwaga na kutafuta mwanamke mwingine na ameshaanza kumtambulisha kwa mashabiki katika mitandao ya kijamii.

Amber Lulu anasema kuwa kama ni kweli kuhusu tetesi hizo basi Prezzo atakuwa amemkosea heshima sana kwa sababu alikuwa ameshamueka moyoni na tayari alikuwa ameshaanza kumtambulishwa kwa baadhi ya ndugu zake.

download latest music    

Akikiri kuwa ameshasikia taarifa za kutambulishwa kwa mwanamke mwingine Amber Lulu akiongea na moja ya gazeti pendwa kutoka GPL, anasema kuwa  kitendo hicho  kama ni kweli basi mwanaume huyo amemdhalilisha sana.

hilo la kutambulisha mwanamke mwingine nimelisikia sana,lakini kama ni kweli amemtambulisha mwanamke mwingine basi  atakuwa amenikosea sana kwa sababu  yeye alikubali nimtambulishe mpaka kwa ndugu zangu na nikafanya hivyo na nilishamweka rohoni.

Amber Lulu na Prezzo walianza kuonekana pamoja mwaka jana(2018) na baadae waliamua kuweka wazi swala laola mahusiano kwa mashabiki wao na kusema kuwa wanategemea kufunga ndoa na wala hawataachana lakini mambo yamekwenda ndivyo sivyo na sanii huyo kutoka kenya ameonekana kuwa na mwanamke mwingine katika viwanja tofauti huko kwao.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.