Loading...

Anerlisa Aanika Siri Yake Iliyompunguza Kilo 49

February 12, 2019 at 10:21
Anerlisa Aanika Siri Yake Iliyompunguza Kilo 49

Mpenzi wa Msanii wa Bongo fleva Ben Pol, Anerlisa Mugai ambaye anatokea nchini Kenya Amefunguka na kuweka wazi Siri Yake iliyomsaidia kupungua kilo 49.

Anerlisa aliibua mjadala mzito nchini kwao Kenya baada ya kupotea katika Mitandao ya kijamii kwa mieiz Tisa alipokuwa mnene na kuibuka akiwa mwembaba na aliyepunguza zaidi ya kilo 49.

Loading...

Katika mahojiano yake na vyombo mbalimbali vya habari, Anerlisa mwenye ukwasi mkubwa akitajwa kumiliki kiwanda cha maji ya kunywa alifunguka na kuianika ratiba yake iliyompa mafanikio makubwa:

Katika miezi miwili ya mwanzo nilipotaka kupungua nilikuwa ninafanya mazoezi mazito kwa muda wa saa moja kila siku. Mazoezi haya yalijumuisha kutembea na mazoezi ya mwili ya kujikunja (yoga).

“Miezi minne iliyofuata nilifanya mafunzo ya matumizi ya viungo kwa msaada wa mwanajeshi mstaafu. Hapa ndipo nilipopoteza uzito mkubwa wa kilo 30 kwa miezi hiyo minne kisha kilo 17 miezi mingine iliyofuata.

“Niliendelea na mafunzo hayo ambapo huwa ninatumia saa moja kila siku kwa ajili ya mazoezi”.

Mimi mwenyewe niliamua kusitisha kabisa matumizi ya sukari. Situmii vitu vya sukari kabisa. Niliamua kuwa ninapikia mafuta ya olive ambayo hayanenepeshi tofauti na mafuta mengine. Napendelea vyakula vya kuchemsha au kukausha kama nyama. Huwa ninapima kiwango cha ‘kabohaidreti’ kwa kijiko cha chai. Pia ninakunywa maji mengi hadi lita tano kwa siku. Napendelea vyakula vya protini kama maharage kwani ukila kidogo tu hushibisha kwa muda mrefu bila madhara ya kusababisha unene.

“Nakula sana mboga aina ya sukuma wiki na spinachi kwa wingi kwa ajili ya kupata vitamini”.

 

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…