Loading…

Aslay Aomba Hasifananishwe Na Alikiba

October 12, 2017 at 09:18
Aslay Aomba Hasifananishwe Na Alikiba

Msanii ambae kwa sasa hivi anafanya vizuri sana kwa katika kazi zake za muziki na amekuwa akiongoza kwa kutoa ngoma mpya kila siku na kupokelewa vizuri na mashabiki  wake amawataka mashabiki wake kutompambanisha na msanii mwenzie Alikiba au msanii yoyote ambae yeye anaona hajamfikia kiwango chake.

Katika mitandao ya kijamii  kumekuwa na tabia ya baadhi ya mashabiki kuweka mipambanisho ya wasanii mmoja na mwingine kitu kilichotokea pia kwa Alikiba na Aslay ambapo watu wanataka kuona ukali wa msanii Alikiba na msanii Aslay katika kutoa ngoma na je ni msanii gani anapendwa na mashabiki wengi,hata hivyo msanii huyo ameombwa kutokufananishwa na msanii alikiba kwa sababu kiwango chake na kiwango cha msanii Alikiba viko tofauti sana.

Loading...

Akiongea na eNews ya EATV,Aslay anasema hata kama yeye kwa sasa anafanya vizuri lakini bado hawezi kufananishwa na msanii mkongwe kama alikiba ambae amekuwa mkongwe katika game kwa muda mrefu , kazi yake imekuwa ikionekana kimaifa lakini pia hata kipaji chake akiwezi kufananishwa na cha msanii alikiba ambae tayari alishapitia mambo mengi katika muziki na bado ana mambo mengi ya kujifunza kwa msanii mkubwa kama Alikiba.

“sio kitu kizuri kwa upande wangu kwa sababu alikiba kazi yake inaonekana na anafanya vizuri,kwahiyo ukisema  unanipamabnisha  mimi na alikiba itakuwa sio picha nzuri na sio  alikiba tu bali hata msanii yeyote msinipambanishe naye, ambaye tayari yupo level zingine” anasema Aslay

Aslay ambae kwa sasa anakuwa akifanya vizuri na vibao vyake vipya kama Pusha, Baby ,Likizo na hichi kipya cha Natamba amekuwa msanii aliyeshika kasi na amekuwa akifanya vizuri katika majukwaa.Aslay ambae kipaji chake kimeanza kuonekana tangu akiwa bado mdogo na baadae akaanza kuimba kwatika band ya Ya Moto Band,yeye ndie alikuwa msanii ambae alikuwa akionekana nyota kuliko wasani wengine.ingwa kwa sasa band aliyokuwa akifanyia kazi kuvunjika bado Aslay ameweza kuasimama peke yake na kuendelea kufanya vizuri zaidi kuliko wenzake wote.

Comments

  1. Aslay mbona mtu mzima,ana mawazo mazur sana

  2. Ndo maana utazidi kutamba maana uko safi

  3. Umewaweka vizuri sana dogo hawana la kusema

  4. Kila la kheri Aslay

  5. Utakuja kuwa msanii mkubwa sana siku zijazo

  6. khalidi bongwajr : November 16, 2017 at 12:34 pm

    Uko vizuri Aslay na kua na msimamo huo ila endelea kuwapa changamoto wakubwa zako safii sana

  7. msimamo mzuri

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment
Loading...

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.