Loading…

Aslay apagawisha jukwaa la fiesta Arusha,nyimbo zake zote zaimbwa.

September 11, 2017 at 20:54
Aslay apagawisha jukwaa la fiesta Arusha,nyimbo zake zote zaimbwa.

Ikiwa imepita siku moja tu tangu tamasha la fiesta lizinduliwe rasmi tarehe 9 septemba ,mkoani Arusha ambapo tamasha ilo hujumuisha wasanii wengi wakubwa na wachanga  nchi Tanzania na hata nje ya nchi,msanii kutoka Tanzania aliyekulia kwenye muziki tangu akiwa na umri mdogo ameacha historia ya kuliteka na kulitawala jukwaa .Msanii huyo ambae kwa sasa anatamba na kibao chake kipya cha “pusha”.

Aslay  hivi karibuni amefululiza kutoa nyimbo nyingi,na licha wa upya wa nyimbo izo bado mashabiki wake walionekana kuimba nyimbo zote tena bila kumpa nafasi msanii huyo kuiba na kipaza sauti,mashabiki walionekana kuwa na mzuka wa kila nyimbo alikuwa anaianzisha kitu kilichamfanya Aslay kushindwa kabisa kuimba muda mrefu,lakini hii ni dalili tosha kuwa msanii Aslay amekuwa akikubalika na kufatiliwa na mashabiki wake kwa ukaribu sana.Aslay alisikika akiwaambia mashabiki zake kuimba hadi kiitikio huku mashabiki wakionekana kuwa na shangwe la kutoka katika kila wimbo aliimba hadi wimbo mpya uliotoka hivi juzijuzi wa pusha.

Loading...

Hata hivyo kwa hivi karibuni Aslay ameonekana kulitawa vizuri jukwaa na kupokea shangwe za kutosha kutoka kwa mashabiki wake akiwa jukwaani mfano mzuri ni katika tamasha la hivi karibuni la  usajili wa  tigo fiesta na show ndogo iliyoandaliwa mkoani Mtwara na kituo cha television cha clouds Tv show  inayojulikana kama ‘jiwe la mwezi’  yenye lengo la kutoa zawadi kwa msanii alifanya vizuri kwa mwezi huo,huku mashabiki wakionekana kumpa sapoti kubwa alipokuwa jukwaani.

Hongera kwake bwana Aslay tunaamini mafanikio haya yataendelea kwa show zote za fiesta zijazo na matamasha mengine pia.keep it up!

Comments

  1. Umetisha sana kaka

  2. We noma Mdogo wangu ila mziki mzuri unajiuza cku zote

  3. Aslay mungu anakuona unajua si kwakukimbiza huku hongera sana Mdogo wangu

  4. Utafika mbali sana kikubwa work hard pray hard

  5. Hatar sana wanyooshe

  6. Umeua dingi mtoto

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment
Loading...

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.