Loading…

Aslay Azungumzia Wasiwasi Aliokuwa Nao Kufanya Kazi Mwenyewe.

October 12, 2017 at 10:53
Aslay Azungumzia Wasiwasi Aliokuwa Nao  Kufanya Kazi Mwenyewe.

Msanii anaefanya vizuri sasa katika muziki Aslay amefunguka na kuongelea wasiwasi aliokuwa nao kipindi anaanza kufanya muziki peke yake bila kuwa chini  ya Mkubwa Fella.Aslay ambae alianza muziki wake akiwa  na umri mdogo sana na wimbo wake wa kwanza wa  naenda kusema kwa mama akiwa chini y ameneja wake  Mkubwa Fella, baada ya muda meneja huyo alitengeneza band ambayo pia Aslay alikuwepo .

Hata hivyo baada ya kukaa katika band zaidi ya miaka mitatu , kundi ilo lilikuja likavunjika huku hakuna sababu ya msingi inayosemwa na mtu yoyote kutoka katika uongozi wa kundi ilo na kufanya Aslay sasa kuanza kufanya kazi zake.Hata hivyo Aslay amefunguka na kusema kuwa  baada ya kuvunjika kwa kundi aliwaza kuanza kazi peke yake lakini alikuwa na wasiwasi mkubwa sana kwani aliamini kuwa bila kuwa na mkubwa hatoweza kufanya kitu chochote katika muziki na akawaza kufanikiwa, lakini baadae alikuja kupata moyo baada ya kuongea na meneja wake mpya anaejulikana kwa jina la Chambuso na kuanza kufanya kazi mwenyewe.

Loading...

‘Nilikuwa na wasiwasi sana kama tutaweza kusonga bila kuwa na mkubwa nyuma yetu,au menejiment yoyote nyuma yoyote,lakini baada ya hapo nilimtafuta Chambuso na yeye akaniambia kuwa tutaweza  kusonga mbele,hivyo tupige kazi,  na kweli tukaanza kupiga kazi na ninakumbuka yimbo yangu ya kwanza  ilikuwa inaitwa angekuona nilianza kuifanya peke yangu na  niliiachia katika tv na radio  mbalimbali,huo ndo wimbo unaonigusa  kutoka moyoni sana kwa sababu unaongelea maisha yangu  halisi kabisa“Aliongea Aslay

Aslay alikwa katika kundi la Ya Moto chini ya manejementi ya Mkubwa Fella na Chambuso lakini baadae kundi hilo lilikuja likavunjika ivyo kusababisha wasanii wote kusambaratika, hata hivyo wapo baadhi ya watu katika mitandao waliokuwa wakisema kuwa wasanii hao hawataweza kuendela vizuri katika muziki kwa sababu alikuwa akiwasimamia kimuziki ambae ndie Mkubwa Fella ndie alikuwa akilimudu kundi ilo lakini maneneo hayo yamekuja kuonekana ni tofauti baada ya Aslay kuweza kufanya kazi peke yake.

Kama ilivyo kawaida kwa mashabiki huwa hayakosekani ya kuongea ndivyo ilivyo kwa sasa kwamba inawezekana Aslay kuwepoa katika band ilikuwa inabana na kuficha kipaji chake, lakini baada ya kutoka ndio kazi na juhudi zake zinaanza kuonekana.

Comments

  1. Angekuona mzigo mkali sana

  2. Kutokata tamaa ni kitu muhimu

  3. Kila wimbo unaotoa ni bomu wewe ni balaa

  4. Wasikufananishe na mtu..hauna mfano kwa sasa

  5. Mola yuko na wewe zidi kutamba

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment
Loading...
wavatar

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.

Aslay Azungumzia Wasiwasi Aliokuwa Nao  Kufanya Kazi Mwenyewe.

Msanii anaefanya vizuri sasa katika muziki Aslay amefunguka na kuongelea wasiwasi aliokuwa nao kipindi anaanza kufanya muziki peke yake bila kuwa chini  ya Mkubwa Fella.Aslay ambae alianza muziki wake akiwa  na umri mdogo sana na wimbo wake wa kwanza wa  naenda kusema kwa mama akiwa chini y ameneja wake  Mkubwa Fella, baada ya muda meneja huyo alitengeneza band ambayo pia Aslay alikuwepo . Hata hivyo baada ya kukaa katika band zaidi ya miaka mitatu , kundi ilo lilikuja likavunjika huku hakuna sababu ya msingi inayosemwa na mtu yoyote kutoka......

Continue Reading