Aslay na Nandy Wazungumzia Wimbo Wao Uliorudiwa Zaidi ya Mara Moja.

Wasanii wanaofanya vizuri pamoja tangu walipoanza kuimba kwa kushirikiana wimbo wa kwanza wa Mahabuba na sasa wametoa wimbo mpya wa Subral kheri mpenzi Nandy na Aslay leo wamezungumzia wimbo huo ambao umetoka jana katika ofisi za Clouds Media.

Wasanii hao wawili waliamua kutoa wimbo huo kwa kuurudia kwa mara ya pila ambapo mara ya kwanza wimbo huo uliimbwa na bi  nasma hamis kidogo .na  wazo la kuurudi lilitolewa na boss wao.

download latest music    

Akiongea katika Power Breakfast Aslay anasema kuwa ‘huu wimbo wa subral kheri  ni mali ya culture Group  lakini huko nyuma kidogo ulishawahi kuimbwa na msanii wa taarabu bi nasma hamis kidogo , hivyo sisi tumeurudia kwa mara ya pili.

Lakini pia Nandy aliweza kuiongelea video ya wimbo huo ambayo imetoka ikiwa local sana “idea ya kutoa nyimbo katika mazingira yale alinipa aslay hata katika wimbo wangu wa kivuruge, hii ni kwa sababu nimepata majibu amzuri ya wimbo wa kivuruge ndio maana hata hii nilikubali kuifanya katika mazingira yael ingawa ilinipa ugumu katika kuuvaa uhalisia.”

Kwa upande wa Aslay yeye anasema kuwa alipokuwa Ya Moto Band alikuwa chini ya watu hivyo ilikuwa rahisi kusema anataka kufanyiwa sehemu yoyote video lakini sasa hivi anafanya mwenyewe ndio maana ameamua kurudi kule uswahilini ambapo yeye mwenyewe ametoka na anashukuru sana kwa sababu watu wanazipokea vizuri, endapo watapata ela kwa kujichanga changa wataaenda kutoa video nje.

Akiongeleaa  kuhusu  maneno yanayosambaa kuhusu bifu lake na msanii mwenzake Ruby, andy amekanusha maneno hayo na kusema kuwa watu wamekuwa wakiongea vitu vya uongo kuhusu wao lakini ukweli ni kwamba wao wako vizuri na kwa sababu wote wanafanya kazi sehemu moja ni vigumu sana kugombana.

Hata hivyo Nandy anasema kuwa wanaweza kutoa wimbo na Ruby siku yoyote ile kwa sababu wote ni watoto wa nyumba moja, na kitendo cha kuwafananisha au kuwagombanisha sio kitu kizuri na hakiwezekani. hivyo watu wasikae wakitangaza na kuzusha vitu ambavyo havina ukweli.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.