Aunt Ezekiel aeleza sababu hatoweza kumrudia mwanaume aliyemuoa miaka 4 zilizopita

Image: Aunt Ezekiel

Baada ya mpenzi wa Aunt Ezekiel wa kitambo Sunday Demonte kurejelea Tanzania kutoka Dubai baada ya kutumikia kifungo cha miaka kadhaa, Aunt Ezekiel amesema kuwa hawezi mrudia mwanaume huyu.

Aunty Ezekiel

Akizungumza kwenye mahojiano na Risasi Mchanganyiko Aunt Ezekiel alisema;

download latest music    

“Ngoja niulize, hivi jamani mbona watu siyo waelewa? Nani asiyejua kama mimi niko na mtu hivi sasa? Na ninaamini kabisa hata yeye (Demonte) anajua? Kwa hiyo hata kama ameachiwa huru na akaja, ukweli utabaki kuwa ndiyo huohuo tu, kwamba tayari nina mtu mwingine maana hata yeye asingeweza kusubiri muda wote huo, hivyo ajue tu hana chake,”

Aliendelea kuongeza kuwa Sasa hivi hawezi kumuacha Mose Iyobo kwa sababu wakona mtoto na maisha yake yamesonga.

Staa huyo aliongeza kuwa, kwa hivi sasa ni vigumu kuachana na mzazi mwenziye aliyenaye kwa kuwa tayari wana mtoto ambaye anapenda kuwaona wakiwa pamoja, hivyo hawezi kumuacha Mose Iyobo. Aunt alisema;

“Hebu fikiria, mtoto wangu amezoea kutuona pamoja mimi na baba yake na ni kitu ambacho anakipenda sana, sasa kwa nini nimuumize?”

 

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua