Aunty Ezekiel Afungukia Tetesi Za Kufungwa Kwa Pub Yake Kisa Kodi

Muigizaji wa Bongo movie na Mfanyabiashara maarufu Aunty Ezekiel amefungukia tetesi za kufungwa pub yake Baada ya kushindwa kulipia kodi.

Kumekuwa na tetesi kwenye Mitandao ya kijamii kuwa Pub ambayo ilikuwa inamilikiwa na Aunty Ezekiel iliyopo maeneo ya Kinondoni imefungwa kutokana na mwanamama huyo kukosa kodi.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Aunty alisema siyo kwanza amefunga Pub yake kwa sababu ya kudaiwa kodi bali eneo hilo anataka kufanya biashara nyingine na hiyo ya pub ataihamishia sehemu nyingine.

Kwa nini nidaiwe kodi wakati nina biashara nyingine nafanya na zinaenda vizuri? Watu huongea vitu ambavyo hawavijui kabisa, nafanya marekebisho ili niweke biashara nyingine na hii nitaihamishia sehemu nyingine”.

Mbali ya Aunty Ezekiel kumiliki Pub hiyo Lakini pia anamiliki sabuni ya Murua ambazo amesema zinauza vizuri sana.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.