Loading...

Aunty Ezekiel Ajibu Tetesi Za Kumwagana na Iyobo

January 11, 2019 at 08:13
Aunty Ezekiel Ajibu Tetesi Za Kumwagana na Iyobo

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Aunty Ezekiel amefungukia tetesi za Kumwagana na baba Watoto Wake ambaye ni mcheza shoo wa Diamond Platnumz, Mose Iyobo.

Katika siku za karibuni kumekuwa na uvumi mwingi ambao umekuwa ukisambaa kuwa wawili hao hawaonekani pamoja kama zamani kwa sababu Penzi Lao limefika ukingoni.

Loading...

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la DIMBA Jumatano, Aunty Ezekiel amesema kuwa hata ikitokea ameachana na Iyobo itabaki kuwa siri yao Lakini kwa sasa wapo vizuri tu.

Wapo wengi wanaamini sisi hatuwezi kudumu, lakini nataka niwathibitishie kuwa mapenzi yetu yapo salama sana, tumejiwekea mikakati yetu ili kuhakikisha tunaishi kama tunavyotaka na si kama wengine wanavyotaka na hata ikitokea tukiachana naamini itabaki siri ya sisi wawili“.

Aunty Ezekiel amesema moja ya mipango yake kwa sasa ni kuongeza mtoto kwa kuwa ni wakati sahihi kwake na mwenzake kufanya hivyo, kama ambayo walikuwa wamepanga toka awali.

Share

Comments

  1. Tumechoka

  2. Hizi story zinaboo sana

  3. Hivi hamna story zingine nyinyi za kusaidia wananchi?

  4. Usijali. Mtaachana tu

  5. Nawaombea sana mwenyezi Mungu awape subra na amani kwenye ndoa yenu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…