Loading...

” Avril hana talanta ya kuimba!” Msanii wa bongo AT amchana Avril

July 13, 2017 at 19:04
" Avril hana talanta ya kuimba!" Msanii wa bongo AT amchana Avril

Msanii wa muziki kutoka bongo anayefanya muziki wa miondoko ya mduara nchini, AT hivi karibuni alidai kuwa mrembo Avril kutoka Kenya hapaswi kuwa akifanya muziki kwa sababu hana talanta.

Avril

Muimbaji huyo anayetoka zanzibar alisema hayo kupitia cloudsfm huku akisema wengi wanamsifia Avril ilhali yeye huimba vibaya. AT alidai kuwa ashawai kufanya kazi na mrembo huyo lakini ilibidi amfute kwenye wimbo wake baada ya kuimba vibaya. Alisema,

 “Nilishaenda ogopa Dj kufanya wimbo na Avril lakini Avril aliimba utumbo mtupu mimi nilimtoa. Avril sio msanii sio kabisa yani sio msanii ambaye unategemea kumsikia halafu unamkuta kama vile alivyo Linah…no yani she very fake kabisa yani mpaka nimeshangaa nilikuwa najua jina lake ni kubwa anauwezo mkubwa lakini nimeenda kufanya nae wimbo aisee ni shughuli mpaka nimemtoa nimemuweka Alice wa THT na ngoma imekuwa kali lakini sijaitoa”

Aliendelea kwa kusema kuwa anachotambua kwenye muziki ni sauti ila sio ukubwa wa jina la msanii.

Leave a Reply

Be the First to Comment!

avatar
wpDiscuz

in Entertainment
Loading...
I write entertainment stories as well review and critic local music. Apart from my busy schedule you can catch me on social pages by clicking on them below