Baada ya Adhabu Kutoka Kwa Naibu Waziri,Pretty Kindy Akiri Kujifunza Kitu.

Msanii wa muziki wa bongo fleva na muigizaji pia Susan Michael maarufu kama Pretty Kindy amefunguka na kusema kuwa baada ya kupewa adhabu na Naibu Waziri wa habari,sanaa na michezo Mh. Juliana Shonza siku kadhaa zilizopoita zimemsaidia na kumfunza kitu katika maisha yake.

Msanii huyo alikuwa amekumbwa na kibano cha kufungiwa kazi zake kwa muda wa miezi sita kwa kosa la kuchapisha picha na kutengeneza video za nyimbo wakiwa nusu uchi kwa madai ya kuwa kufanya hivyo ni kukiuka na kuvunja maadili ya Taifa.

download latest music    

Pretty Kindy amemwambia mwandishi wa habari kuwa tangu afungiwe na kupewa adhabu hiyo ameamua kubadilika na kuamua kuanza kuvaa nguo za heshima kwa sababu alichogundua ni kwamba kuvaa nguo za utupu kunamvunjia heshima na kuna mpotezea hadhi yake katika jamii inayomzunguka hivyo ameamua kukubaliana na hali halisi na ameamua kukaa kimya.

Kwa upande mwingine ameamua kunipa funzo kubwa sana maishani mwangu,tangu nimepewa ile adhabu yaani hata ukikutana na mimi utagundua kwa kile ninachokisema.nimebadilika sana na ninavaa nguo za heshima sana sasa, nimegundua nguo za nuzu uchi zinakufanya udharaurike na kukupotezea heshima.

Pretty Kindy alikuwa msanii wa kwanza kuitka wito wa Naibu Waziri na kupewa adhabu yake akaikubali na kujutia tukio ilo ingawa mapokeo ya adhab hiyo yaliuwa tofauti hata kwa mwenzie Gigy Money.Ambapo msanii hyo baada ya kupewa adhab yake alionyesha kujutia kosa lake na kukiri kuwa ni kosa na akaweka ahadi ya kuanza kubadilika lakini kwa upande wa wasanii wengine kama sanchi hakutokea kabisa katika ofisi za Baraza kuitikia wito lakini Gigy Money alisema kuwa huko ni kunyima uhuru wa wasanii,

Swala hilo la mavazi kwa wasanii limekuwa likipokelwa tofauti kwa wadau wa sanaa huku wengin wakiona ni sawa na wengi wakiona kama bado kuna vitu Baraza wanatakiwa kuliweka sawa kabla ya kuwafungia wasanii.

Hata hivyo Baraza kwa kushirikiana na Naibu waziri bado wamekuwa wakitilia mkazo swala hilo kwa wasanii wote na endapo wataendelea nalo basi wao kama viongozi hawataacha kulitilia mkazo na kuchukua sheria.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.