Baada Ya Kudai Kuwa Kwenye Mahusiano na Godzilla, Bella Adaiwa Kuvishwa Pete na Mwanaume Mwingine

Msanii wa Bongo movie Isabella Mpanda alitengeneza headlines wiki iliyopita Baada ya kudai kuwa kwenye mahusiano na Aliyekuwa Msanii wa Bongo fleva Marehemu Godzilla.

Mbele ya Media mbali mbali Bella alilia machozi na kusema kuwa Mpaka kipindi Godzilla anafariki dunia yeye Ndiye alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na msanii huyo.

download latest music    

Gazeti la Risasi Jumamosi,  lilizungumza na rafiki wa karibu na Bella ambaye alionesha kushtushwa na kitendo cha Bella kujitambulisha kwamba alikuwa na uhusiano na marehemu wakati miezi michache iliyopita alichumbiwa na mwanaume mwingine aitwaye John aliyejaliwa kuzaa naye mtoto mmoja.

Kwenye mahojiano na Gazeti hilo Bella alidai kuwa alishaachana na mwanaume aliyemchumbia takriban miezi mitano iliyopita na baada ya kuachana naye, aliamua kurejea kwa Godzilla ambaye aliwahi kuwa mpenzi wake kabla ya kuchumbiwa.

Niliachana na baba mtoto wangu nikaamua kurudi kwa mpenzi wangu wa siku nyingi ambaye ni Godzilla hivyo ndivyo ninavyoweza kusema kwa sasa, naomba uniache maana nipo kwenye majonzi”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.