Loading...

Baada Ya Ndoa Yake Kuvunjika, Mbunge Bonnah Kaluwa Azima Tetesi Za Kufumaniwa

March 01, 2019 at 10:49
Baada Ya Ndoa Yake Kuvunjika, Mbunge Bonnah Kaluwa Azima Tetesi Za Kufumaniwa

Mbunge wa Jimbo la Sergerea (CCM) Bonnah Kamoli, ameweka wazi kuwa hajawaji kufumaniwa na aliyekuwa mumewe kama jinsi watu wanavyozungumza na kusisitiza kuwa kama yupo mwenye ushahidi juu ya hilo autoe.

Bonnah amelazimika kujibu tuhuma hizo za ikiwa ni siku chache tangu akiri kuachana na mume wake, Mosses Kaluwa hali iliyomfanya yeye kubadilisha majina yae ya mwisho katika taarifa zake ikiwemo mitandao ya kijamii.

download latest music    

Tuhuma hizo za fumanizi zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii huku wengine wakienda mbali na kusema kwamba sababu za kuachana na mume wake ni kutokana na kufumaniwa Jijini  Dodoma.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Bonnah ameandika maneno haya :

Wahenga wanasema jambo likiongelewa sana bila majibu linaweza kugeuka likawa kweli. Sasa ni hivi mimi Bonnah Ladisus Kamoli au jina langu lingine Neema sijawahi kufumaniwa hata siku moja katika maisha yangu”.

Sio kwamba mimi ni muadilifu sana au malaika ila hapakuwepo na mtu wa kunifumania nadhani mtakua mmenielewa na sitaongea tena na kama kuna mtu anaushahidi alete na kanifumania na nani”.

Loading…

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment