Baada ya Seduce me ya Alikiba kufikisha 2M YouTube, Christina Shusho amuandikia King Kiba ujumbe huu

Image: The artist Alikiba during the MAMA 2016, in Johannesburg, South Africa on October 22nd, 2016

King Kiba anaonekana kuwa yeye ndiye Mfalme Wa Nyimbo za bongo na hii ni baada ya msanii huyo kuachia wimbo wake mpya Seduce me ambao umefikisha milioni 2 siku tatu baada ya kuiwachia.

Mashabiki wake pia wameonekana kupenda wimbo huu ikiwemo Wema Sepetu na wengine Kama muimbaji wa nyimbo za injili, Christina Shusho. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Christina alionyesha mapemzi yake kwa wimbo huu wa King Kiba kwa kuandika;

download latest music    

“Leo unaweza kukuta mtu kaitwa kanisani aongoze wimbo wa sifa halafu akalianzisha Seduce Me, Eeh jamani Kiba we noma, wimbo ni mzuri sana kitaaluma kama anavyopenda kusema bosi Ruge. Hauna picha za aibu , naweza kuuangalia nikiwa na familia, labda sijui maana ya Seduce Me. Timu Kigoma Wamanyema oyeeeee. Cha mwisho Ali Kiba basi siku nyingine tutembelee kanisani ukiwa mfalme huchagui dini wote wako”

Hata hivyo kwa sasa ameweka rekodi mpya ya kuwa msanii wa kwanza Afrika Mashariki kufikisha 2 Million view YouTube na siku tatu.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua