Baada ya Siri ya Kuzaa na Weru Kuvuja’Natamani Raisi Magufuli Azime Data”;-Steve Nyerere

Msanii wa bongo movies Steve Nyerere amefunguka na kusema kuwa endapo atapata bahati ya kuonana na raisi atamshauri kufunga mitandao ya kijamii kwa sababu imekuwa inachosha sana, kutokana na mambo yanayoongelewa katika mitandao hiyo.

Steve Nyerere amesema kuwa anatamani sana Tanzania kufuata mfumo wa China wa kufungua mitandao na kutumia mitandao maalumu kwa ajili ya kutangaza mambo ya kiuchumi na wala sio kusambaza habari za uongo na umbea isiyokuwa na ukweli  wowote.

download latest music    

bado tunahitaji kuwa na mfumo kama wa China, nitafurahin sana siku magufuli akizima data nchini,nadhani mheshimiwa anahitaji kushauriwa kwa hili kwa sababu kama tunataka kujenga Tanzania ya viwanda basi  siku moja tuzime data hata mwezi lazimatutafikia malengo tena andka kabisa kwa herufi kubwa Nyerere anataka kukutana na Magufuli  amnongoneze kuhusu data azime tu hata mwezi ili watu wafanye kazi.

Steve anasema kuwa asilimia90 ya wau wanaoishikatika mitandao wamekuwa wakifanya kazi zisizoingizia pesa taifa lakini wamekuwa wanatunga tu maneno ya uongo na kisha kuona ndio kazi zao za kutwa nzima.

Hivi karibuni kulisambaa picha za msanii huyo na mwanadada weru sengo na kuvuja kwa siri kuwa wawili hao wamekuwa na mahusiano ya muda mrefu kufikia kupata mtoto mmoja ambae mwaka huu may ametimiza mwaka mmoja.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.