Baada ya Wema Kunimwaga Nilichanganyikiwa- Idris

Mshindi wa Big Brother 2014 na mchekeshaji maarufu Idris Sultan amefunguka kwa mara nyingine kuhusiana na mahusiano yake maarufu na Mrembo Wema Sepetu. Idris na Wema walikuwa kwenye uhusiano kwa muda na kuachana mapema mwaka jana wamekuwa kwenye vichwa vya  habari mara kwa mara na hata baada ya wao kukiri kuachana kwao mashabiki wao wamekuwa wakiwaomba warudiane.

Idris na Wema waliachana mara baada ya kutangaza kuharibika kwa ujauzito wa Wema  uliokuwa na miezi michache ambapo baadae walikuja kuweka wazi kuwa ujauzito ule ulikuwa wa mapacha wawili wa kike. Huku wakiwa hawajaweka rasmi sababu ya wao wawili kuachana watu wengi kwenye mitandao ya kijamii walitunga ya kwao.

download latest music    

Katika mahojiano aliyafanya Idris hivi karibuni aliweka wazi kuwa Wema ndio aliyemuacha yeye yaani “alimwaga” na kumuacha ambapo alifunguka kuwa kile kitendo kilimuumiza sana na kumfanya aumie sana na kufikia hatua ya kutembea na wasichana wengi ili mradi ajaribu kumsahau Wema, ambapo alitembea na wanawake zaidi ya thelathini (30) ili ajaribu tu kuziba pengo lililoachwa na madame na aweze kumsahau na kuendelea na maisha yake.

Idris amefunguka na kusema kuwa sasa wamekuwa washkaji tu huku wakisapotiana katika mambo mbalimbali kama yeye alivyoenda kwenye uzinduzi wa filamu yake ni kwasababu ni marafiki wa karibu na sio wapenzi tena.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.