Baba Kanumba Atuma Ujumbe Mzito Kwa Lulu

Baba mzazi wa aliyekuwa staa wa Bongo movie Steven Kanumba, Charles Kanumba ‘Baba Kanumba’ ameibuka na kudai kuwa anamsaka Elizabeth Michael ‘Lulu’ ili ampe ujumbe wake.

Siku chache Baada ya Lulu kumaliza kifungo chake, Baba Kanumba amesema anamsaka Lulu ili aweze kumpa nasaha zake kama baba pamoja na ujumbe aliopewa na babu wa Kanumba.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi, Baba Kanumba alifunguka kuwa siku chache kabla Lulu hajamaliza kifungo, alitokewa na babu wa Kanumba yaani baba yake mzazi ambaye alifariki wakati mwanaye Kanumba anazaliwa na kupewa jina lake.

Babu wa Kanumba alinitokea na kuniambia nimkumbushe Lulu atekeleze mambo ya kimila ambayo nimewahi kumwambia tena ya kwenda kaburini kwa Kanumba na kufanya usafi na kumuombea na hapo atakuwa ameondokana na kile kivuli cha marehemu.

Wakati Lulu anafanya hayo anatakiwa awepo ndugu wa upande wa ukoo wa Kanumba ili kushuhudia na akimaliza hayo atakuwa yupo salama na hatapata mikosi tena kwenye maisha yake na kile kivuli cha Kanumba kitakuwa kimemuondoka lakini vinginevyo atapata taabu”.

Lakini Mzee Kanumba alisema hamlazimishi Lulu kufanya hayo mambo na pia amekiri kuwa hana kinyongo na Lulu hata kidogo na kumtakia kila la kheri maishani.

Sina kinyongo na Lulu, nimefurahi sana yeye kumaliza kifungo na ninamuombea mafanikio makubwa sana kwenye maisha yake, ninahitaji na ninamsaka sana kwa udi na uvumba maana nina mengi ya kumwambia kama mwanangu”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.