Baba Levo Atoa Tahadhari Kwa Nuh Mziwanda na Nedy Music juu ya Shilole

Ikiwa ni siku kadhaa tu zimepita tangu msanii wa muziki bongo Zuwena maarufu kama Shiloleh kufunga ndoa, aliyekuwa Mc katika harusi yao ambayo ilifungwa mwaka jana na haruis kufanyika mwaka huu January 14 amefunguka na kuwataka wasanii wenzake ambao walikuwa na mahusiano na Shiloleh kutulia na kuacha usumbufu kwa mwanamke huyo kwa sababu alishaolewa na hawezi kurudiana nao tena.

Baba Levo ameswataja wasanii hao kuwa ni Nedy Muisc  pamoja na Nuh Mziwanda ambao walikuwa wana mahusiano na Shiloleh hapo mwanzo kabla ya shiloleh kuwa na uchebe ambae ameamua kufunga nae ndoa.

download latest music    

Baba Levo amewaambia wasanii hao kuwa watumie kigezo cha kimapenzi yao ya nyuma kuwa karibu na Shiloleh kwa sababu sasa hivi shiloleh ni mke wa mtu na endapo watakuwa wanaonekana kunyapia nyapia kwa shiloleh watapigwa makofi na uchebe.

na kuanzia sasa hivi shiloleh naomba utulie na kumuheshimu mume wako ambae umeamua kuanza nae maisha , na kwa hiki kinachotokea sasa hivi naomba nedy music na nuh mziwanda muache kumfatilia shiloleh uchebe amekomaa atatupiga makofi, atawapiga makofi na biashara inaishia hapo.

Shiloleh alishawahi kuwa na mahusiano na wanaume hao kipindi cha nyuma kabla ya kuolewa na uchebe ambapo kwa upande wa nuh mziwanda amekuwa akimsumbua na kumkebei Uchebe hata baada ya kutangaza kufunga ndoa na Shiloleh.

Wasanii wengi wamekuwa wakitilia mkazao swala la wanaume wa nyuma wa mwanadada huyo kumuacha Shiloleh kufanya maisha yake mapya ya ndoa yawe ya amani huku wengi wao wakiwataaharisha kumuogopa Uchebe ambae anaonekana kuwa mkali.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.