Babu Seya na Papi Kocha Kuwaanda Mashabiki Kwa Ujio Mpya.

Wasanii wa muziki wa dansi baba na mtoto wake wameanza kuwandaa mashabiki wao kukaa mkao wa kula kwa ujio wap mpya na kutoa ahadi ya kuwa kazi zinazokuja zitakuwa nzuri kuliko hata zile zilizokuwa zikitolewa hapo mwanzoni.

Wasanii hao hivi sasa wameanza maandalizi ya ujio wao mpya wa nyimbo zao baada ya miaka 14 ya kukaa gerezani na kazi zao kuwa zimesimama kwa muda wote huo na kuwaacha mashabiki wao wakiwa na hamu kubwa ya kazi zao.

download latest music    

Akizungumza katika photo shoots zao mpya kwa ajili ya kazi yao inayokuja, Papii Kocha alisikika akisema”miaka 14 sio mchezo  mambo kama haya nimeyamiss , niliyamiss sana nimemiss vitu vingi, picha kama hivi mambo haya kule hakuna kabisa, lazima uelewe kuwa hii ni dunia nyingine.

Papi Kocha anasema kuwa mashabiki wao wakae mkao wa kula kwa sababu  sasa hivi  wana mpango wa kutoa nyimbo nzuri zaidi ya zile za zamani.kwa kuwa tumejipanga nyimbo zinazokuja ni nzuri zaidi  ya zile tulizokuwa tunafanya hapo mwanzoni.

Wasanii hao ambao ni wanafamilia walipewa msamaha wa raisi siku ya tarehe 9 Desemba mwaka 2017 wakiwa ni moja ya watu waliopokea msamaha wa raisi siku hiyo.Hivi karibuni naibu waziri wa habari ,sanaa na michezo aliwakutanisha wasanii hao na uongozi wa Wanene Entertainment  kwa ajili ya kuwasimamia waweze kufanya nyimbo zao.

Wasanii hao walihukumiwa kifungo cha maisha baada ya kukutwa na hatia ya kulawiti watoto.Hata hivyo  wasanii hao kabla ya kutolewa walishawahi kutuma ujumbe kwa raisi Magufuli na kuomba msaada  na kukiri kuwa walishajifunza kwa miaka waliokaa jela.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.