Babu Tale Aachiwa Huru Rasmi

Mkurugenzi wa kampuni ya Tip Top Connection na Meneja wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Babu Tale ameachiwa huru rasmi baada ya kusota rumande kwa Siku mbili.

Tale alifikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar, juzi Jumatano Mei 23, 2018 kufuatia kesi yake anayodaiwa na Sheikh Hashim Mbonde kiasi cha Tsh. Milioni 250 ambapo kesi hiyo iliahirishwa baada ya hakimu aliyetoa amri ya kumkamata kutokuwepo mahakamani hapo.

download latest music    

Kipindi cha nyuma mahakama hiyo ilimwamuru Babu Tale alipe Sh. milioni 250 Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde, baada ya kupatikana na makosa ya ukiukwaji wa hakimiliki kwa kutumia masomo yake kibiashara bila ridhaa yake kinyume cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki.

Babutale ameachiwa kutoka Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam tangu jana Alhamisi na sasa yupo uraiani japo haijafahamika iwapo yupo nje kwa dhamana au vinginevyo.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.