Baby J aongelea kuhusu ndoa yake kwa mara ya kwanza

Baby J kwa mara ya kwanza ameongelea ndoa yake ambayo ilikuwa ikuzungumziwa sana mitandaoni.

Leo akiwa kwenye Clouds FM alieleza kwa nini hakuwa akiishi na muwewe baada ya kufunga ndoa.

download latest music    

”Wakati najiandaa kusafiri kwenda New York aliko ambako tulipanga mimi na yeye tukaishi, ilitakiwa iwe siku ya 15. Lakini ilipofika siku ya 10 mwenzangu akakamatwa huko aliko. Japo aliniambia kuwa atakamatwa, sijajua nini kilisababisha.

“Wakati anakamatwa ilikuwa saa 10 jioni baada ya muda ule sikumpata tena kwenye simu. Halafu bahati mbaya, mama yake mume wangua alikuwa amakuja Afrika kwa ajili ya harusi, so, nilikuwa niko naye. Bahati mbaya akafariki kwa mshtuko mida ya kama saa 12, na baada ya siku ya pili ndio akanipigia kujua juu ya msiba wa mama yake. Hivi na yeye alikuwa jela ikawa mtihani.

“Tunawasiliana kwa sasa hivi, ila ni mwaka wa tano toka ameshikiliwa. Halafu kipindi mwenzangu anakamatwa, mimi nipo kwenye msiba. Watu wakaanza kunitumia sms wakinisema kuwa tulikuambia, tutaendelea kupishana hapa hapa. Bahati nzuri, mwenzangua alikuwa ameniachia ujauzito mchanga, lakini bahati mbaya uliharibika kutokana na hiyo hali.

“Ninavyowasiliana na mwenzangu, ananisihi sana nivumilie. Nina matumaini japo sitaki kulizungumzia hilo.” Alisema.

About this writer:

Irari Ngugi

Lover of life, lover of big boobs and certified celebrity squasher. Catch me if you can on facebook as Irari Ngugi