Bahati Bukuku Amruhusu Mumewe Kuoa Mke Mwingine

Msanii wa nyimbo za Injili nchini Bahati Bukuku amefunguka na kuweka wazi kuwa ametoa ruksa kwa aliyekuwa mume wake Daniel Basila kufunga ndoa.

Bahati Bukuku amesema kuwa hana tatizo Kama mume wake wa zamani akifunga ndoa tena na mwanamke mwingine kwani wameshapeana talaka kwa muda mrefu sasa.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Bahati Bukuku amesema baada ya kupata habari kuwa mumewe amepata mchumba anayeitwa Elizabeth Ngaiza na wanatarajia kufunga ndoa hivi karibuni hakushtuka kwani aliachana na mumewe siku nyingi kidogo.

Unajua kwanza ndio nazipata habari hizi za mume wangu kuoa lakini sina kipingamizi kwani nilishaachana naye siku nyingi na alinipa talaka rasmi mahakamani Julai mwaka huu, hivyo sioni tatizo kabisa”.

Bahati Bukuku na mume Wake Daniel Basila wametengena kwa miaka zaidi ya 14 sasa na walipeana talaka miaka michache iliyopita.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.