Balaa La Vannesa na Jux Jukwaa La Fiesta,Mapenzi Ni Mubashara.

Wakiwa bado wanakiri kuwa  hakuna mapenzi kati yao wasanii wawili Vannesa Mdee  pamoja na Jux wamewashangaza mashabiki kwa matukio yao ya kuimba pamoja katika matamasha mbalimbali ya Fiesta huku wakionesha kuwa hawana ugomvi wowote ilihali wamekuwa mbali katika mapenzi.wasanii hao ambao hata wamekuwa wakionekana waki-hang out pamoja katika mikoa mbalimbali tofauti na jukwaani wanaonekana kuwa bado na hisia kwa kila mtu kutokana na vile wanavyokuwa wakijiwakilisha jukwaan mbele ya mashabiki.

Tarehe 25, wikiendi iliyopita wasanii hao walipata bahati ya kutumbuiza katika jukwaa kubwa la Fiesta mkoani Dar Es Salaam ambapo waliwashangaza watu wengi baada ya kuimba kwa kuonyeshana mahaba na kuwa karibu zaidi.

download latest music    

Walipokuwa wakiimba mashabiki zao walikuwa wakishangilia na kupiga kelele za kuwataka wawili hao kurudiana, hata hivyo inasemekana kuwa wawili hao bado wanaendeleza mahusiano yao pamoja na kwamba wamekuwa wakikataa kuhusu kurudiana kwao.

Vannesa Mdee ni mmoja kati ya wasemaji katika kukanusha taarifa za kurudian kwao huku wakisema kuwa wamekuwa wasanii na wafanyabiashara kwa uda mrefu hivyo ugomvi wa kimapenzi hauwezi kuharibu kazi na biashara.

Vannesa na jux wakiimba kwa pamoja

Jux akimtengeneza Vannesa cheni kifuani kwake

Wakiwa pamoja jukwaani.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.