Loading...

Baraka Aendelea Kuwatuhumu Uongozi Wa Alikiba

December 07, 2017 at 07:01
Baraka Aendelea Kuwatuhumu Uongozi Wa Alikiba

Msanii anaefanya vizuri na kibao chake cha Sometimes Baraka the Prince, amefunguka na kusema kuwa kuna kipindi uongozi wa msanii alikiba walikuwa wakimfanyia figisu kwa ma-DJ ili wasicheze nyimbo zake katika media mbalimbali ili kuweza kumdidimiza.Hata hivyo msanii huyo anasema kuwa pamoja na kwamba walikuwa wakifanya kwa siri lakini alikuwa akiambiwa na baadhi ya watu hao kwa sababu alikuwa akiongea nao vizuri na walikuwa hawapendezwi na kitu hicho.

Kuna baadhi ya DJ’s walikuwa wakiambiwa wasicheze nyimbo zangu wengine mpaka walikuwa wakipewa ela kwa ajili tu ya kutokupiga nyimbo zangu lakini ndo hivyo unakuta Dj anakufata  anakwambia unajua nimeambiwa nisipige nyimbo zako na ela nimepewa kabisa .

Kwaio hicho ni kitu cha kushukuru kwa sababu watu wangekuwa hawanipendi na siongei nao vizuri kama inavyoenezwa sidhani kama kuna mtu angewza kunifuata na kuthubutu kuniambia  taarifa kama hizo kabisa .This means napendwa na watu na tayari nina Empire yangu tayari.

Baraka the Prince amekuwa akisema kuwa uongozi uluipita wa Rock400 umekuwa ukimfanyia michezo mibaya mara tu baada ya kuondoka katika uongozi huo huku wakitaka afe kimuziki, hii sio mara ya kwanza kwa baraka kutoa lawama kwa uongozi huo na baadhi ya watu maarufu katika kiwanda cha muziki kuhusu kumrudisha nyuma katika muziki.

Loading...

Baraka the Prince na Alikiba walikuwa katika menejiment moja ya Rock400 inayopatikana nchi south afrika lakini msani Baraka the Prince aliamua kujiondoa huko na kufanya kazi zake.Hata hivyo baada ya kuamua kufanya kazi mwenyewe alijikuta akiingia katika migogoro na baadhi ya watu katika muziki huku akimtuhumu kila aliyehisi ni mbaya wake kwa kuhususha muziki wake.

 

 

Leave a Reply

avatar

in Entertainment

Loading…

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.