Loading...

Baraka The Prince Ahofia Kuachia Ngoma Mpya Kisa Kombe La Dunia

July 11, 2018 at 08:42
Baraka The Prince Ahofia Kuachia Ngoma Mpya Kisa Kombe La Dunia

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Barakah The Prince amefunguka na kuweka wazi kuwa hawezi kuachia ngoma mpya kwa sasa pamoja na kuwa mashabiki zake wanamtaka afanye hivyo.

Baraka The Prince amefunguka na kudai kwa sasa kuna matukio mengi ambayo yamekuwa yakiendelea kwa mfano jambo kubwa kwa sasa ni Kombe la dunia.

Loading...

Barakah amekaa kimya kwa muda mrefu bila ya kuachia ngoma yoyote ile kwa kipindi sasa kiasi cha mdahabiki zake kumfuata Kwenye mitandao ya kijamii na kumuulizia ngoma mpya.

Ambapo amekiri kuwepo kwa matukio mbali mbali kama misiba na na bifu ya wasanii wengine mbali mbali au hata wasanii wengi kuachia ngoma kwa wakati mmoja husababisha ngoma kufeli sokoni.

Lakini Baraka amedokeza ujio wa ngoma yake mpya itakayoitwa ‘Sina’ ingawa hajaweka wazi kuwa ngoma hiyo itatoka lini lakini itakuwa mara baada ya Kombe la dunia kuishia.

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…