Barakah Adai Baada Ya Kusoma Biblia na Quran Ameamua Kuwa Muislam Ili Kuwa Karibu na Mungu

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Barakah The Prince amefungukia uamuzi wake wa kubadilisha dini kutoka kuwa mkristo na sasa kuamua kuwa Muislamu.

Barakah amedai kuwa maamuzi hayo ya kubadilisha dini hawakuwa ya ghafla bali yalichukua  muda mrefu hadi kuyatekeleza.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, amesema kuwa amejitahidi kusoma Biblia na Quran na akaja kubaini kuwa Uislamu ndio dini yake pekee kwa sasa ambayo itamuweka karibu na Mungu.

Baada ya kusoma biblia sana na kusoma Quran sana kukawa kuna vitu nikawa nimeipenda dini ya kiislamu Lakini pia naamini Mungu ni mmoja na tunamuamini Mungu mmoja tofauti ni dini tu”.

Lakini pia Barakah ameweka wazi kuwa pamoja na kubadilisha dini na kuwa Muislamu na kuupenda zaidi Uislamu lakini bado anasoma biblia kwani anataka kumjua Mungu zaidi na kuwa karibu naye.

Siku za nyuma baada ya Barakah kubadilisha dini na kuwa muislamu kuna tetesi zilidai kuwa alibadili dini kwa ajili ya mpenzi wake Naj ambaye ni Muislam taarifa ambazo Barakah alizikataa.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.