Loading...

Barakah The Prince Afungukia Tetesi Za Kufilisika

December 19, 2018 at 07:40
Barakah The Prince Afungukia Tetesi Za Kufilisika

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Barakah The Prince amefunguka na kuongelea tetesi zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefilisika.

Tetesi hizo zimezidi kupamba Moto sasa hivi kwa sababu Barakah ameonekana kukonda kupita maelezo hali iliyopelekea wengi kufikiria huenda ni kwa sababu ya maisha magumu.

Loading...

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha XXL ya Clouds Fm, Barakah amesema kuwa yeye hajawahi kuwa tajiri na hivyo kwasasa ndio ameanza kuitafuta hela yake kwa kuanza kufanya kazi zake mwenyewe huku akidai kuwa yeye sio msanii wa kuweka maisha yake hadharani.

Mimi ni mmoja ya wale artist sipendelei   sana kuweka hadharani hali  ya uchumi wangu au maisha yangu na ndio maana ni vigumu mtu kujua kama niko sawa Kiuchumi au nimeshuka Kiuchumi kwasababu nina Personal life so naamini pia pesa inatautwa nikiitafuta inakuja na inaweza yakatokea matatizo ikatumika labda vibaya”.

Na sio kama tatizo kubwa sana kwasababu hata makampuni makubwa huwa yanayumba, matajiri wapo wengi kuliko hata mimi na mimi sijawahi kuwa tajiri labda nimefilisiki sijawahi kuwa na hela mimi sasa hivi ndio nataka labda niitafute hela sasa now ndio naenda kuitengeneza hela yangu, kwanza niko nafanya kazi zangu mwenyewe kwasababu mi sio yule artisht wa kuonyesha maisha yangu”.

 

Share

Comments

  1. Pole

  2. Mbona mimi naona ako sawa tu

  3. yataka galby

  4. jameni hayatuhusu

  5. apambane na hali yake

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…