Barnaba amjibu aliyekuwa mke wake kupitia ujumbe huu wa Instagram?

Barnaba na aliyekuwa mke wake wameonekana kupashana kupitia mitndao yao ya Instagram. Hii ni baada ya mrembo huyo aliyekuwa mke wake ambaye pia ni mzazi mwenziye, kuposti picha akiwa na mpenzi wake wa sasa mitandaoni huku akiandika ujumbe unaoelezea sababu za ndoa yao kuvunjika.

download latest music    

Hata hivyo Barnaba naye aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram huku akiwasifia wanawake – lakini mashabiki wake wanaonelea kuwa alikuwa anamjibu mke wake.

Alindika kusema;

“Mama aliniambia ukimtukana mwanamke basi umenitukana na mimi, siku zote nawaona kama mama zangu, hongera wanawake wote duniani, salamu zangu juu yenu Jumapili ya leo nawapenda sana, na wale mliopoteza mama zenu fanyeni ibada juu yao waweze punguziwa adhabu ya kifo au kufutiwa kabisa, Bwana Yesu asifiwe sana Jumapili ya Mungu tumpe Mungu Wakristo wenzangu”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua