Barnaba Awaongelea Wasanii Wanaofeli THT .

Msanii mwenye kipaji ambacho akijawahi kushuka tangu aanze muziki wa Bongo Fleva Barnaba Elias anaejulikana kwa jina  la Barnaba Classic amefunguka na kuwaongelea baadhi ya wasanii ambao walikulia kimuziki katika jumba la sanaa la THT na kushindwa kuendelea kimuziki.Barnaba akiwa kama mmoja wa wasanii waliolelewa na kukua katika jumba la sanaa la THT amekuwa ni mmoja wa wasanii wa kuigwa kutokana na mafanikio yake aliyonayo mpaka saivi katika muziki.

Barnaba ambae amekuwa maarufu kwa uandishi wa baadhi kwa nyimbo za wasanii wengine wengi kwa sasa amekuwa msanii mwenye mafanikio mpaka kufikia hatua ya kufungua studio yake mwenyewe inayojulikana kama High Table Sound akiwa producer mwenyewe.

download latest music    

Barnaba anasema kuwa anawashangaa wasanii ambao walikuwa wote katika tasnia ya muziki na walikuwa wote katika malezi ya kimuziki THT lakini kwa sasa wameshindwa kabisa kuendeleza sanaa iyo tangu watoke THT. kwake yeye anaamini kuwa waliotoka THT kwa mbinde ndio walioshindwa kuendelea kimuziki kwa sababu wameondoka kwa wivu na kisirani hivyo hawataweza kufanikiwa kwa sababu wameshindwa kukumbuka shukrani ya vitu walivyokuwa wakipewa katika jumba ilo.

Akiongea na eNews ya televisheni ya EATV Barnaba anasema “wapo wajanja waliovuna tunda la THT , THT ni tunda,  na ni msingi ambao mpaka saivi bado unaendelea kuleta watu wastaarabu ,wapo wengi walioondoka kwa jealous,upumbavu na kutokuthamini shukrani   wametoka  THT na wakashindwa kuendeleza sanaa wamepotea ” anasema Barnaba.Hata hivyo Barnaba ametaja wasanii wenzie wa THT ambao wanafanya vizuri katika muziki wakiwa nje ya THT ni pamoja na Estelina Sanga”linah”, Mwasiti, Amini

Akiwa kama mmoja wa wasanii waliosota sana kimuziki mpaka kufika pale walipofikia Barnaba ambae saivi hana menejementi na ametoka THT anafanya vizuri na nyimbo zake mpya alizotoa hivi karibu  wa “tunafanana” na  “mapenzi jeneza”, ukiachana na muziki Barnaba amebahatika kuwa na mtoto mmoja aliyezaa na mwanamke aliyekuwa nae kwa muda tangu anaanza muziki lakini walikuja kuachana hivi karibuni na kuamua kutengana na mwanamke huyo.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.