Barnaba Aweka Wazi Siri Ya Sauti Yake

Akiwa kama mmoja wa wasanii wanaofanya vizuri sana katika kazi zake zz musiki na sasa hivi anatamba na kibao chake cha mapenzi jeneza,msanii Barnaba Elias Maarufu kama Barnaba  Classic kipaji kikubwa kutokaTHT  amefunguka na kuongelea moja ya siri zake kubwa katika kutunza sauti yake ambayo imekuwa adimu sana katika muziki wake.

akiongea katika Clouds E ya Clouds Tv alipokutwa katika mazoezi ya kujitayarisha kwa ajili ya kufanya mazoezi ya kuperfom katika shoo ya mwisho ya tamasha la Fiesta, Barnaba amesema kuwa  kila anapojua kuwa anatarajia kufanya shoo sehemu amekuwa akijitahidi sana kutunza sauti yake ili aweze kufanya vizuri katika  shoo zake.

download latest music    

Barnaba ambae ni msanii anaesifika kwa kuweza kufanya live band kwa muda mrefu na mara nyingi zaidi katika show zake anasema kuwa amekuwa akifanya mazoezi, amekuwa akijitahidi kupumzika sana na hata kupunguza swala la kufanya mapenzi ili kuweza kumtain nguvu zake.

litu kikubwa uwa nazingatia kupumzika muda mwingi na kuwahi kulala,nalala muda mwingi sana hili kupumzika kwa sababu show ninayoenda kuifanya ni kubwa sana, lakini pia najitahidi kutokula vyakula vya wanga kama mahindi, maharage, mtama maana hivyo ni vyakula vinavyoweza kuacha mabaka kooni na kusababisha sauti kutoka kwa shida na kukuumiza koo, lakini pia najitahidi sana kunywa maji mengi na kwa wingi zaidi ya kawaida.Kitu kikubwa pia nazingatia sana katika kufanya mazoezi ya mwili kama kukimbia na kupiga push-up kwa sababu ya kutafuta pumzi maana kuimba muda mrefu kunahitaji pumzi sana.Lakini katika vyote ninaweza nisifanye mapenzi hii wiki nzima mpaka show ipite.Wasanii kutunza sauti jukwaani ni kama wachezaji wa mpira tu.

Barnaba na wasanii wengine wanategema kukonga nyoyo za watu novemba 25 , katika jukwaa la Fiesta katika uwanja wa Leaders Club jijini Dar Es Salaam baada ya tamasha hilo kuzunguka kwa zaidi ya mikoa 16 na kuamua kumalizikia jijini hapo.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.