BASATA Wakanusha Tetesi Za Kumuita Wema Sepetu

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limekanusha tetesi za kumuita na kumhoji staa wa Bongo movie Wema Sepetu baada ya kusambaza Mtandaoni picha na video zenye utata.

Wiki iliyopita Wema alizua gumzo baada ya kuachia picha na video za yeye na mpenzi wake huku video ikiwaonyesha wawili hao wakiwa wanapeana mabusu moto moto na picha ikiwaonyesha wakiwa chumbani.

download latest music    

Mwishoni mwa wiki iliyopita kuna tetesi zilisambaa kuwa kutokana na picha hizo chafu Wema Sepetu ameitwa na BASATA kwa ajili ya kufika katika ofisi zao taarifa ambazo kwa saaa BASATA wamezikataa.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Afisa Habari BASATA, Agness na kukanusha taarifa hizo huku akidai kama mwanadada huyo anaenda Basata ni kwa mambo yake binafsi sio kwamba aliitwa.

Sio kweli Wema ameitwa Basata, hata sisi tunasikia hizo habari na kuihusisha na mambo yake ya kwenye mitandao, sisi kama Basata atu-deal na maisha binafsi ya wasanii labda afanye tukio katika kazi ya sanaa ndio tunaweza kumuita,Kama ni mambo ya mtandaoni TCRA ndio wenye mamlaka”.

BASATA ni sehemu ya wasanii, ni wazazi wa wasanii, kama anakuja sisi tutampokea na kuzungumza naye hukusu sanaa yake na namna ya kujiweka kama msanii lakini mpaka sasa hatuna taarifa kama anakuja lakini akija sawa tutampokea”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.