BASATA Wampongeza msanii AT Kwa Kutwaa Tuzo

Baraza la sanaa la Taifa  limeonyesha ushiriki wake katika kukuza sanaa kwa kumpongeza moja ya wasanii wakongwe nchini  AT baada ya kushinda tuzo mbili kwa mkupuo katika tuzo za Mama Awards zilizofanyika wiki iliyopita nchini Marekani na kufanya msanii kutoka nchini nyakue tuzo hizo.

AT alishinda tuzo hizo katika kategoria mbili tofauti yaani  International   Artist na Best  Music Video. Hata hivyo kwa kuonyesha pongezi hizo na kutaka watu waendelea kujua kuhusu habari hizo  BASATA waliposti video hizo katika ukurasa wao wa instagram na kuandika salamu za pongezi hizo.

download latest music    

Mwanamuziki  maarufu katika miondoko ya mduara  nchini Ally Ramadhani, kwa jina la kisanii kama AT, ameshinda tuzo mbili za MAMA AWARDS huko nchini Marekani. Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kama mlezi wa wasanii nchini  linampongeza kwa dhati msanii AT  kwa heshima na  sifa kubwa walioipatia Taifa, huko ughaibuni. Aidha BARAZA linapenda kuchukua nafasi hii  kuwasihi wasanii wengine nchini  kuongeza ubunifu na ubora zaidi  kwenye kazi zao ili sanaa yetu iweze kufika mbali  zaidi kimataifa.

Wiki  ambayo msanii huyo alichukua tuzo pia ndio ilikuwa wiki  wasanii wawili aliyochukua tuzo msanii Alikiba pamoja na Nandy ambao pia waliiwakilisha vizuri tanzania huku nchi nigeria katika yuzo za AFRIMA.hii inaonyesha kuwa wasanii wa tanzania kwa sasa wameanza kuwa chachu ya kukuza musiki wa tanzania na kuweza kujulikana kwa nchi za nje.pongezi nyingi ziwafikie kwao.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.