Ben Pol Akana Tetesi za Yeye Na Barnaba Kuunda Kundi Moja

Msanii wa Bongo fleva Bernard Paul maarufu kama Ben Pol amefunguka na kuzima tetesi zilizosambaa Kwenye mitandao ya kijamii na kudai kuwa yeye na Barnaba wanaenda kundi moja la muziki.

Barnaba na Ben Pol ni moja kati ya Wasanii Kwenye tasnia ya Bongo fleva ambao wana ukaribu sana na wameshafanya nyimbo kadhaa pamoja.

download latest music    

Siku za hivi karibuni waliwaambia mashabiki zao wanataka kuunda kundi moja na kufanya Muziki pamoja ambapo kundi hilo walipanga kuliita BEBA yaani kirefu ni Ben na Barnaba.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Wasafi Tv, Ben Pol amekana taarifa na kusisitiza kuwa walivyosema hivyo ilikuwa ni utani lakini hawakumaanisha kama kweli walikuwa wana mpango wa kuwa kundi moja:

BEBA was a a joke tulisema kwa nini wasanii wanaungana wawili wawili hlafu wanakata vifupi vya majina yao kwanini na sisi tusifanye hivyo? Lakini ilikuwa kama utani ingawa tumesharekodi nyimbo kama mbili lakini hatifanya kama kundi bado lakini huwezi kujua huko mbele because we are family na tunasopitiana”.

Wasanii mbali mbali wamekuwa wakiungana na kuwa kundi moja mfano ni Rostam ambao ni Roma na Stamina na MoCo ambao ni Moni na Country Boy.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.