Bifu Jipya Laibuka Kati ya Wema Sepetu na Batuli

Waigizaji wa Bongo movie nchini Wema Sepetu na Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ waliowahi kuwa marafiki wazuri hapo zamani na kisha kutibuana kisa fedha za kampeni za CCM walizopiga kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, wameibuka tena na bifu hilo jipya.

Warembo hao waliokuwa na ukaribu na urafiki uliopitiliza hadi kufikia hatua ya kuvaa nguo sare urafiki wao uliingiwa na dosari mapema mwaka huu na kupelekea urafiki huo kuvunjika. Lakini toka wamemaliza urafiki huo kumekuwa na maneno ya chini chini ambayo wamekuwa wakirushiana.

download latest music    

Batuli aliyekuwa kimya kidogo kwa miezi hii aliibuka na kusema kuwa Wema Sepetu hawezi kutamba kwenye filamu pasipo kuwepo marehemu Kanumba. Batuli ameyasema hayo mara baada tu ya Wema kuachia filamu yake mpya inayoitwa ‘Heaven sent’ aliyoifanya na mwigizaji mwenzake Gabo. Wema aliyeingizwa na kwenye sanaa na marehemu Kanumba na kutoanaye  filamu kadhaa zilizofanya vizuri sokoni.

Wema ni moja kati ya supastaa anayeongoza kwa kubadilisha marafiki kwani amekuwa na urafiki na wasanii wengi kama Kajala ambaye aligombana naye baada ya Kajala kumuibia Wema mwanaume, Kuna Auntyezekiel ambaye urafiki wao uliisha baada ya Aunty kuanzisha urafiki na Zari ambaye ni hasimu wa Wema na rafiki yake wa mwishoni alikuwa Munalove lakini naye pia walitifuana baada kumkamata uchawi na kumtuhumu kuwa alikuwa anamuonea wivu.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.