Bifu la Nandy na Ruby Lamalizika.

January 12, 2018 at 16:17
Bifu la Nandy na Ruby Lamalizika.

Siku za nyuma ilikwa ikisemekana kuwa msanii Ruby na mwanadada mwenzie Nandy wamekuwa na bifu zito hasa kwa upande wa Ruby ambae amekuwa akimsakama Nandy kuwa amekuwa akitembelea gap lake alilikuwa ameliacha kwa muda mrefu tangu atoke katika muziki na ndio maana ameweza kufanikiwa katika kazi hiyo.Hata hivyo Nandy hakuwahi kujibu kitu chochote kuhusu tetesi hizo zaidi ya kukaa kimya na kumuacha msanii huyo akiendelea kuongea na kusema kuwa yeye ni bora zaidi kuliko mwenzie.

Hata hivyo siku za karibuni msanii Ruby alipokuwa katika interview aliambiwa aimbe wimbo mpya wa Nandy unao-trend sana kwa sasa unaojuliakna kwa jina la kivuruge na aliweza kuimba kwa hisia na kwa kuupatia kabisa.

Loading...

Baada ya video hiyo kusambaa sana katika kurasa nyingi za instagram,Nandy aliamua pia kuweka video hiyo na kuonyesha shukrani zake kwa msanii mwenzie  wa kike.

Alichokiandika Nandy baaada ya kuposti video ya Ruby akiimba wimbo wake.

Nandyy akionyeshwa kufurahishwa na kusema kuwa wamekuwa akim-inspire sana lakini pia hawashindwi kufanya kazi pamoja na ikawa ni moja ya project nzuri.Hata hivyo Nandy amesema kuwa watu waache kusikiliza maneno na kuyazusha bila kuwa na uhakika.

hata hivyo baada ya ruby kutafutwa na kuulizwa hakuweza kupatikana lakini kwa upande wa ruby alisikika akisema .nimefurahi sana kuona ruby anaimba wimbo wangu  najua sana,unajua sisi hatujawahi kuwa na bifu ila hayo uwa yanazushwa tu na watu.tarajieni kuona makubwa huko mbeleni kwa sabau tunafanya kazi sehemu moja, kwaio hata tukiamua kufanya kazi kwa pamoja kama mashabikiwanavyoshauri ni sekunde tu.-Aliongea Nandy kwa simu akionyesha furaha yake.

 

6
Leave a Reply

avatar
6 Comment threads
0 Thread replies
0 Followers
 
Most reacted comment
Hottest comment thread
1 Comment authors
IbrahimDavidsonJessicaLuluEmily Recent comment authors
newest oldest most voted
Rose
Guest
Rose

Wafanye kazi pamoja sasa

Emily
Guest
Emily

Wadada wamefanya vizuri sana beef hazina maana

Lulu
Guest
Lulu

Kesi kwisha sasa mziki utambe

Jessica
Guest
Jessica

Wote wazuri kwa kuimba

Davidson
Guest
Davidson

Hongera sana kwao

Ibrahim
Guest
Ibrahim

Safi sana


in Entertainment
Loading...

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.