Bifu La Young Dee Na Dogo Janja,Chanzo ni Muna

Kwa muda sasa kumekuwa na chokochoko kati ya wasanii wawili wa muziki wa Bongo Fleva yaani Young Dee na Dogo Janja ambapo katika kufatilia sababu inaonekana ni yale maneno ambayo Young Dee aliyaongea yaliyokuwa yanamuhusu Dogo Janja na Young Killer Msodoki kuwa yeye (Young Dee) ni mkubwa kimuziki hivyo hataki kabisa kusikia watu wakimfanisha na wasanii hao wawili ambao kwake anawaona bado wachanga hawajamfikia kiwango chake. Young Killer alinyamzaza na hajaonekana kuongea chochote kuhusu ili lakini Dogo Janja hakuweza kuvumilia na kuamua kujibu maneno ya Young Dee na kumwambia kuwa hata yeye hawezi kulinganishawa  msanii kama yeye ambae anavuta unga, kabisa hawezi kuongea na ‘mteja’.

Bifu limeendelea na kuwa kubwa mpaka baadhi ya wasanii waliamua kuingia nakuwashauri kuyamaliza mambo hayo, kati ya wasanii hao ni pamoja na Nikki wa Pili.Lakini jana msanii wa muziki wa singeli Sholo Mwamba nae aliamua kufunguka kuhusu bifu ilo huku akiamua kumwaga ubuyu hadharani kuhusu sababu ya wasanii hao kugombana ni mwanamke.

download latest music    

Akiongea na eNews ,Sholo Mwamba ambae alikuwa chini ya menejiment ya Muna Entertainment alifunguka na kusema kuwa kwa sasa yeye na Muna hawafanyi kazi pamoja na sababu sio kwamba yeye alichokwa na Muna bali yeye alimchoka Muna, alipoulizwa sababau ya yeye kumchoka meneja wake alijibu “Kitu ambacho mimi kiliniuzi na nilikichoka kwa Muda ni kitendo cha sisi wanaume kufanya kazi na kutafuta ela  afu tukienda pale  kwa muna tunakuta madogo wengune wamekaa kwenye makochi wamejiachia, sisi wahuni tunaenda kuimba visingeli vijijini tunaleta mpunga kwa bosi alafu bosi anatumia na wajinga”aliongea Sholo Mwamba

hapo wote vingasti tu, tunawakuta pale kwa bimkubwa wanajiachia achia tu, Dogo Janja, Young Dee, wanagombana wanagombania demu, ila sisi tunakuja kwa bosi tunawakuta hayo mambo ya kugombana ni miyeyusho tu” aliongezea Sholo Mwamba

Hata hivyo Sholo pia anaonekana ana wivu wa mapenzi kwa Muna Love na kufikia hatua ya kusema ” namshangaa bosi si angenipa hata mimi, akinipa sisemi, tunakula kimyakimya”

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.