Bila K-Lyn Labda Ningekuwa Nimeshakufa :-Mengi

Mume wa mwanadada K-lyn amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake labda kama asingekutana na mlimbwende huyo angekuwa ameshakufa mpak sasa kutokana na malezi na mapenzi anayoyapata kutoka kwake.

Mengi akiongea na kituo cha tv cha citizen anasema kuwa watu wanadhani ilikuwa rahisi kumpata mwanadada huyo kwa sababu tu yeye amekuwa akijulikana kama mwanaume tajiri lakini ukweli ni kwamba hakuna kitu kama icho kwa sababu mwanadada huyo alikuwa na msimamo na alikuwa akimkwepa sana.

download latest music    

Mengi anasema kuwa alikuwa akimfatilia sana hata kusafiri kutoka mji mmoja kwenda mwingine pale aliposikia kuwa mwanadada huyo yuko nje na yeye alikuwa nje na walikuwa wakiwasiliana na hata alipomuomba kumuona hakutokea katika maongezi yao.

mengi anasema kuwa baada ya hapo walirudi Tanzania na waliendelea kuwasilina ana ndipo alipokubali kuonana  nae kwa mara ya kwanza  wakiwa Tanzania.

Mengi anakiri kuwa haikuwa rahisi kwake kumpata mwanadada k-lyn lakini haimanishi kuwa alifankiwa kwa sababu ya pesa, lakini anasema kuwa kwa anavojiona yee kwa sasa ambapo tayari ana umri wa miaka 75, bila kuwa na k-lynkatika maisha yake inawezekana kabisa kuwa angekuwa tayari ameshafariki siku nyingi.

Jackline Mengi ni moja ya wasichana waliopata mafanikio makubwa sana kutokana na biashara yake ya vitu vya thamani, ambapo hata yeye alipata umaarufu wake na kuutumia vizuri baada ya kushiriki miss tanzania na hata baadae kuwa msanii,.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.